PSEA Katika Mstari wa Mbele – Pamoja Tunakataa

 

Together we say no to sexual exploitation and abuse

Kampeni ya kimataifa ya lugha nyingi ya kuongeza ufahamu juu ya ulinzi dhidi ya unyanyasaji na dhuluma za kijinsia (PSEA) miongoni mwa wafanyakazi walio mstari wa mbele. Pamoja tunaKATAA! unyanyasaji na dhuluma za kijinsia. 

  • Muhtasari wa maelezo: ENFRSP na AR
  • Jinsi ya Kuongoza: EN,FR,SP, na AR
  • Nyenzo zote katika lugha 22 HAPA

Shirika la Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) kwa ushirikiano na Watafsiri Wasio Mipaka (TWB) walianzisha kampeni ya kimataifa ya kuwawezesha zaidi wafanyakazi na washirika walio mstari wa mbele katika mapambanao dhidi ya unyanyasaji na dhuluma za kijinsia (SEA). Mradi huu unalenga wafanyakazi wa nyanjani ambao wana jukumu muhimu katika programu za usaidizi na hutagusana zaidi na wafadhiliwa na wanajamii. Chini ya kaulimbiu “Pamoja Tunakataa”, PSEA katika mradi wa Mstari wa Mbele hutoa kifurushi cha kina cha lugha nyingi cha nyenzo za uhamasishaji kilichoundwa ili kuwapa wafanyakazi na washirika hawa wa mstari wa mbele maarifa ya PSEA ili kusaidia kuzuia SEA kutokea na vilevile kuongeza ufahamu katika kutambua na kuripoti SEA.

Mradi wa Mstari wa Mbele wa PSEA umebuniwa kupitia mkabala wa chini-juu ambao ulitumia maoni ya zaidi ya wafanyakazi wa mstari wa mbele 3,000 wa shughuli za uhisani kutoka zaidi ya nchi 80 ili kuhakikisha ufaafu na ufanisi wa nyanjani wa bidhaa na ujumbe wa mradi. Kwa kutumia mifano hai ya PSEA na maudhui rahisi, kifurushi cha uhamasishaji cha kampeni kinajumuisha nyenzo za uchapishaji zenye michoro, jumbe za sauti na rasilimali za medianuwai zinazopatikana katika zaidi ya lugha 20. Pia upimaji wa nyenzo ulifanyika katika nchi tano: Afghanistani, Bangladeshi, Columbia, Sudan Kusini na Uturuki.

Bidhaa zote zilizotengenezwa zinapatikana kwa matumizi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa, washirika na jamii pana za PSEA kwenye tovuti ya IASCHAPA.

Lugha

Kiamharic, Kiarabu, Kibahasa, Kibambara, Kibangla, Kidari, Kiswahili cha DRC, Kiingereza, Kifaransa, Fulfulde, Krioli cha Haiti, Kihausa, Kiarabu cha Juba, Kilingala, Lugha ya Myanmar, Kinepali, Pashto, Kireno, Kihispania, Kiswahili, Kitigrinya, na Kituruki.

Seti teule za zana pia zimechaguliwa kutumiwa katika mwitikio wa Ukraine na zinapatikana katika lugha za Kiukreni, Kipolandi, Kiromania, Kirusi na Kislovaki.

Aina za Rasilimali

  • Nyenzo zilizochapishwa zenye vielelezo vingi
  • Ujumbe wa sauti
  • Vifaa vya midia-anuwai

Marekebisho

Bidhaa zinapatikana katika umbo la mwisho, hata hivyo, mashirika yanakaribishwa kuongeza jina/nembo zao kwenye nyenzo zilizochapishwa. Zaidi ya hayo, mashirika yanaombwa kuongeza maelezo muhimu ya mawasiliano ya eneo hilo kwa ajili ya kuripoti katika nafasi iliyotolewa. Marekebisho haya yanaweza kufanywa kwa njia ya vibandiko au ujumuishaji wa kisanduku cha matini katika hati za PDF. Kwa mwongozo wa jinsi ya kuongeza kisanduku cha matini kwenye hati za PDF, na maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia nyenzo hizi tafadhali tazama How To Guide.(EN,FR,SP,AR)

Tafsiri

Kwa usaidizi wa kutafsiri bidhaa hizo katika lugha ambayo tafsiri yake haipo, tafadhali wasiliana na: PSEA-SH@iom.int au wfp.psea@wfp.org.