IOM inafafanua ulaghai kama uwasilishaji visivyo au ufichaji wa ukweli wa mambo kwa nia ya kudanganya na kupata manufaa yasiyoidhinishwa. Unahusisha vitendo vya kimakusudi na vya udanganyifu, kama vile kughushi hati yoyote kwa nia ya kupata manufaa, kama vile pesa, mali au huduma. Uwasilishaji visivyo unaweza kuwa uwasilishaji wa uongo, ufichaji, au kutofichua.

Kwa kawaida, kuna vipengele vinne vinavyohusika katika kesi yoyote ya ulaghai: (1) taarifa isiyo ya ukweli ambayo (2) inatolewa kimakusudi huku mtoaji akijua kwamba ni ya uongo, (3) kutegemea taarifa ya uongo ya mwathiriwa, ambayo husababisha (4) hasara kwa mwathiriwa. Mwathiriwa anaweza kuwa mtu, au linaweza kuwa shirika, kama vile IOM.

Ulaghai mwingi unaweza kugawanywa katika kategoria tatu, kila moja ikiwa na vijikategoria:

  • Taarifa za ulaghai: za kifedha na zisizo za kifedha
  • Matumizi mabaya ya mali: kuchukua pesa taslimu, orodha ya vitu au mali zingine za IOM; kutoa ankra kwa vifaa au kazi zisizokuwepo; mishahara kwa wafanyakazi wasiokuwepo.
  • Ufisadi: kufanya jambo kwa nia ya kupata faida isiyostahili. Mara nyingi ufisadi hutokea walaghai wanapotumia ushawishi wao kimakosa katika shughuli ili kujinufaisha wao wenyewe, au mhusika mwingine ambaye hafai kunufaika, kutokana na mgongano wa maslahi, hongo, kiinua mgongo haramu, au upokonyaji wa kiuchumi

Aina za ulaghai zilizoorodheshwa hapo juu si zote. Mwenendo wowote usiofaa au unaofanana au unaohusiana nao au kitendo chochote cha kuhimiza, kuficha, kula njama au kushirikiana kwa hila katika mojawapo ya vitendo vilivyo hapo juu pia huchukuliwa kuwa ulaghai.

Hapa kuna mifano michache ya visa vya Ulaghai, Ufisadi na Matumizi Mabaya ya Rasilimali katika IOM ambavyo vilisababisha kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu
  • Mfanyakazi aliomba na kupokea rushwa kutoka kwa mchuuzi wa IOM;
  • Mfanyakazi aliomba na kupokea pesa kwa njia ya ulaghai kutoka kwa mfadhiliwa wa IOM kwa kisingizio kisicho cha ukweli;
  • Mfanyakazi alihamisha pesa za awali za matumizi bila idhini inayotakiwa hadi kwenye akaunti ya kibinafsi ya benki ya mfanyakazi mwingine, ambaye alizitumia fedha hizo vibaya;
  • Mfanyakazi alihusika katika utumiaji mbaya wa mali (wizi wa fedha na ubadhirifu) kisha akaghushi saini ya Afisa Mkuu wa IOM katika nchi kwenye hati za fedha za IOM;
  • Mfanyakazi hakufichua uhusiano wake wa kibinafsi (kifamilia) na wafanyakazi wengine, huku akihusika moja kwa moja katika kuajiri na kukuza taaluma ya mojawapo wa hawa;
  • Mfanyakazi alitumia vifaa vya Teknolojia ya Habari vya IOM kufikia, kutazama, kuhifadhi, na kusambaza picha na video zenye maudhui ya ngono;
  • Mfanyakazi aliendesha gari la IOM akiwa mlevi, akiwa kazini, na kubeba watu wasioidhinishwa kwenye gari la IOM.

 

Ni muhimu kukumbuka kwamba wafanyakazi wa IOM hawawezi kufanya kazi kwa uadilifu, kwa kujitegemea na bila upendeleo, katika michakato ambapo maslahi ya kibinafsi yanahusika. Kupambana na ulaghai, ufisadi, na matumizi mabaya ya rasilimali katika IOM ni jukumu la msingi la wafanyakazi wa IOM na kila mmoja wao anao wajibu wa kuripoti mienendo mibaya. Wafanyakazi wa IOM wanaoripoti mienendo mibaya kwa nia njema wana haki ya kulindwa dhidi ya ulipizaji kisasi (tazama https://weareallin.iom.int/sw/ulipizaji-kisasi).

 

Inaweza kuwa vigumu kutofautisha aina mbalimbali za mwenendo mbaya. Huhitaji kujua aina ya mwenendo mbaya ili uweze kuripoti. Iwapo utapata au kushuhudia mwenendo mbaya wowote, makosa au ikiwa unahisi kuwa kuna kosa lililofanyika, unapaswa kuripoti kwa Ofisi ya Uangalizi wa Ndani (OIO) ya IOM kupitia jukwaa la kuripoti mwenendo mbaya la IOM, “We Are All In” (www.weareallin.iom.int) au kwa baruapepe kwa oiointake@iom.int, hata kama huna hakika hiyo ni aina gani ya mwenendo mbaya.


Ilisasishwa mwisho: Machi 2024