IOM ina sera ya kutovumilia kabisa unyanyasaji na dhuluma za kijinsia (SEA) kutoka kwa watumishi na wafanyikazi na watu wengine walioajiriwa na kudhibitiwa na wakandarasi wa IOM. Kutovumilia kabisa kunamaanisha kwamba hatua madhubuti zinaanzishwa ili kuzuia SEA. Hatua zinazofaa za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wafanyakazi wa IOM ambao itabainika kuwa wamekiuka sera husika za IOM. Hatua za kinidhamu, ikiwa ni pamoja na kuachishwa kazi mara moja, zitachukuliwa bila kujali hadhi, aina ya mkataba, au cheo. Kwa waajiriwa wasio wafanyakazi wake, IOM inaweza kusitisha mkataba wa mkosaji. Kushindwa kwa wakandarasi wa IOM kuzingatia majukumu ya kimkataba yanayohusu uzuiaji, ukatazaji, kuripoti na uchunguzi wa SEA kunaweza kusababisha kusitishwa kwa mkataba kati ya IOM na mkandarasi husika.
Sera ya IOM inaeleza kwamba mara nyingi kuna tofauti asili na muhimu ya uwezo kati ya wafanyakazi na wanufaishwa na inaarifu kwamba shughuli za dhuluma na unyanyasaji wa kingono na wafadhiliwa ni marufuku kabisa. Kwa maneno mengine, SEA hutokea wakati watu ambao wana mamlaka wananyanyasa na kudhulumu watu wanaoweza kudhuriwa kwa urahisi kwa madhumuni ya ngono. IOM haitavumilia hali ya kutojali kuhusu SEA.
Unyanyasaji wa kijinsia unamaanisha matumizi mabaya yoyote halisi au yaliyojaribiwa kwa walio wepesi kuathiriwa, wenye uwezo tofauti, au uaminifu, kwa madhumuni ya ngono, ikijumuisha, lakini si tu, kufaidika kifedha, kijamii au kisiasa kutokana na unyanyasaji wa kijinsia wa mtu mwingine.
Dhuluma za kijinsia humaanisha uingiliaji halisi au tishio la kimwili lenye mwelekeo wa kingono, iwe kwa matumizi ya nguvu au hali zisizo sawa au za kulazimisha.
Unyanyasaji au dhuluma za kijinsia hutekelezwa na wafanyakazi wa IOM au wakandarasi wa IOM (kama vile wagavi, watoa huduma au washirika watekelezaji) dhidi ya mtu ambaye si mfanyakazi/mkandarasi wa IOM, kama vile mfadhiliwa. SEA ni tofauti na udhalilishaji wa kijinsia ambao unafanywa na wafanyakazi wa IOM dhidi ya mfanyakazi mwingine wa IOM. Ili kpata maelezo zaidi kuhusu udhalilishaji wa kijinsia, unaweza kutembelea https://weareallin.iom.int/sw/udhalilishaji-ukijumuisha-udhalilishaji-wa-kijinsia.
- Mifano ya Unyanyasaji na Dhuluma za Kijinsia
-
- Ubadilishanaji wa pesa, ajira, makazi, chakula, bidhaa au usaidizi mwingine wa kibinadamu kwa ajili ya ngono, ukijumuisha fadhila za ngono au tabia zingine za kufedhehesha, au kudhalilisha, au kunyanyasa (Unyanyasaji wa kijinsia)
- Kumtisha au kumlazimisha mtu afanye ngono na mtu mwingine au atoe fadhila za ngono kwa mtu mwingine (k.m. wafadhili au wafanyakazi wenzake) katika hali zisizo sawa au za kulazimishwa kwa faida ya mtu mwenyewe (Unyanyasaji wa kijinsia)
- Kutumia huduma za makahaba (Unyanyasaji wa kijinsia)
- Kufanya ngono kuwa sharti la usaidizi (Unyanyasaji wa kijinsia)
- Kumlazimisha mtu kushiriki katika ukahaba au ponografia (Unyanyasaji wa kijinsia)
- Shambulio la kingono (tendo lolote la ngono lisilotakikana au la kulazimishwa lililofanywa bila ridhaa, likijumuisha ubakaji, ulawiti, na ngono ya midomo ya kulazimishwa) (Dhuluma za kijinsia)
- Shughuli yoyote ya ngono na watu walio chini ya umri wa miaka 18, kuwepo au kusiwepo na idhini (Dhuluma za kijinsia)
- Kubusu, kushika, kusugua, au kitendo kingine kisichotakiwa chenye mwelekeo wa ngono (Dhuluma za kijinsia)
- Mahitaji ya wafanyakazi wa IOM
-
- Kuelewa kikamilifu aina ya tabia ambazo zinaweza kuchukuliwa kuwa SEA.
- Kukuza tabia inayoheshimu na kupendelea haki za wanufaishwa.
- Ripoti madai au tuhuma zozote za SEA au kitendo chochote cha kulipiza kisasi kinachohusiana na SEA. Wafanyakazi wa IOM wanaoripoti mwenendo mbaya kwa nia njema wana haki ya kulindwa dhidi ya ulipizaji kisasi (tazama https://weareallin.iom.int/sw/ulipizaji-kisasi).
- Kanuni za kimsingi
-
Ili kulinda wafadhiliwa na watu wanaoweza kuathiriwa kwa urahisi na kuhakikisha uadilifu wa shughuli za IOM, kanuni za kimsingi zifuatazo zinafaa kufuatwa na wafanyakazi wa IOM:
- SEA hujumuisha vitendo vya mwenendo mbaya sana na ni sababu za kusitisha ajira na pia kujumuishwa katika Clear Check.
- Kushiriki ngono na watoto (watu walio chini ya umri wa miaka 18) ni marufuku.
- Ubadilishanaji wa pesa, ajira, bidhaa au huduma kwa ajili ya ngono ni marufuku.
- Mahusiano ya kimapenzi kati ya wafanyakazi wa IOM na wafadhiliwa hayakubaliki na ni marufuku yanapokuwa ya dhuluma au unyanyasaji.
- Sharti wafanyakazi wa IOM waripoti wasiwasi wao kuhusu wafanyakazi wenzao kuhusika na SEA.
- Wafanyakazi wa IOM, hasa walio katika nyadhifa za uongozi, wanalazimika kuanzisha na kudumisha mazingira ambayo yanazuia na kutoa ulinzi dhidi ya SEA.
- Mifano ya visa vya SEA katika IOM ambavyo vilisababisha hatua za kinidhamu
-
- Mfanyakazi alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mfadhiliwa wa IOM mwenye umri mdogo
- Mfanyakazi aliwagusa isivyofaa na kuwatisha wafadhiliwa wawili
- Mfanyakazi hakushirikiana na uchunguzi wa SEA kwa kutotoa taarifa kwa
- Mfanyakazi aliwapa wafadhiliwa pesa ili washiriki naye ngono
- Mfanyakazi alimgusa mfadhiliwa isivyofaa na isivyohitajika wakati wa uchunguzi wa kimatibabu
- Mfanyakazi alijihusisha na unyanyasaji na dhuluma za kijinsia kwa kutumia huduma za makahaba au wafanyabiashara wa ngono.
Inaweza kuwa vigumu kutofautisha aina mbalimbali za mwenendo mbaya. Huhitaji kujua aina ya mwenendo mbaya ili uweze kuripoti. Iwapo utapata au kushuhudia mwenendo mbaya wowote, makosa au ikiwa unahisi kuwa kuna kosa lililofanyika, unapaswa kuripoti kwa Ofisi ya Uangalizi wa Ndani (OIO) ya IOM kupitia jukwaa la kuripoti mwenendo mbaya la IOM, “We Are All In” (www.weareallin.iom.int) au kwa baruapepe kwa oiointake@iom.int, hata kama huna hakika hiyo ni aina gani ya mwenendo mbaya.
Ilisasishwa mwisho: Machi 2024